Nyota anayekipiga ndani ya klabu ya Juvevtus, Miralem Pjanic amegomea dili la kujiunga Manchester United na PSG licha ya habari kueleza kuwa ana mpango wa kusepa ndani ya Juventus kutokana na kukosa nafasi kwenye kikosi hicho.
Awali ilielezwa kuwa anaweza kujiunga na Manchester United kwa kuwa aliwahi kunukuliwa akisema kuwa anahitaji kuchezea ligi kuu ya England ila taarifa zinaeleza kuwa anataka kwenda Barcelona.
Pjanic amejiunga Juventus mwaka 2016 huku akifanikiwa kucheza jumla ya mechi 167 na kutwaa mataji sita makubwa.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.