Home Makala PSG Wababe ,Watinga Fainali

PSG Wababe ,Watinga Fainali

by Sports Leo
0 comments

PSG wamefanikiwa kuibuka wababe na kutinga mazima hatua ya fainali ligi ya mabingwa ulaya baada ya kushinda mabao 3-0 dhidi ya Leipzig mjini Lisbon siku ya jana katika mchezo wa hatua ya nusu fainali uliokuwa na ushindani mkubwa.

Kipindi cha Kwanza cha mchezo PSG ilitupia mabao mawili ambapo bao la kwanza lilipachikwa na Marquinhos dakika ya 13 na Di Maria alifunga bao la pili dakika ya 42 .

Bao la tatu lilipachikwa na Benatti dakika ya 56 kipindi cha pili cha mchezo na kuwaacha nyuma mazima wapinzani wao kwa kutinga fainali ambayo inatarajiwa kuchezwa Jumapili,Agosti 23 dhidi ya mshindi atakayepatikana kwenye mchezo wa Bayern Munich na Lyon.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited