Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Ahmad Ahmad anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye mchezo wa watani wa jadi Yanga na Simba utakaochezwa Machi 8 uwanja wa taif siku ya Jumapili.
Ahmad anatarajiwa kutua nchini Tanzania siku ya kesho ikiwa ni maalumu kwa ajili ya ziara ya siku tatu nchini huku Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania, Clifford Ndimbo amesema kuwa maandalizi ya kumpokea raisi huyo yamekamilika.
“Kila kitu kipo sawa na tunatarajia kumpokea Rais wa CAF ambaye atakuwa mgeni rasmi kwenye mchezo wa Yanga na Simba kwa kuwa aliomba kwa Rais wa TFF, Wallace Karia kuja kuishuhudia mechi hiyo”.alisema Clifford
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.