Aliyekua kocha wa klabu ya Yanga sc Sead Ramovic ameibomoa klabu hiyo kwa kuwachukua watu wawili muhimu katika benchi la ufundi la klabu hiyo.
Ramovic amemuondoa mkurugenzi wa ufundi wa klabu hiyo Abdi Hamid Moallin ambaye anaondoka Yanga Sc na atajiunga na CR Belouizdad ya Algeria ya Kocha Sead Ramovic ambaye ndie aliyependekeza usajili wake.
Mbali na Moalin pia Mpho Maruping ambae alikuwa video Analyst wa Yanga sc ambaye sasa anajiunga na CR Belouizdad, Sead Ramovic, Abdi Hamid Moallin na Mpho wanaungana tena CR Belouizdad.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Hata hivyo kuondoka kwa wataalamu hao kumetokana na kocha mpya wa Yanga sc Roman Folz kuamua kuja na safu yake mpya ya benchi la ufundi ambalo anaamini litafanya kazi yake kama anavyopenda.