94
Kocha mkuu wa klabu ya Yanga Nasreddine Mohamed Nabi tayari ameshakabidhi ripoti kwa uongozi wa klabu kwa ajili ya msimu ujao katika ripoti hiyo kocha Nabi anahitaji kusajili wachezaji 8 wa nguvu ili kuendana na ushindani uliopo kwenye ligi kuu Tanzania Bara (VPL) na mechi za kimataifa msimu ujao.
Katika ripoti hiyo Nabi ameorodhesha wachezaji hao ni golikipa mmoja, mabeki watatu (wa kulia, kushoto na Kati) kiungo mchambuliaji mmoja, winga mmoja na washambuliaji wawili wa nguvu katika wachezaji hao Nabi anataka wachezaji 5 wawe wa kimataifa huku 3 wazawa.
Pia Kocha huyo amependekeza kuachwa kwa wachezaji wanne wa kimataifa na wachezaji watano wazawa Yanga tayari imeanza kusajili baada ya kumalizana na Beki wa kulia wa Djuma Shaban raia wa DRC Congo na Sasa inafanya mazungumzo na wachezaji wengine ili kukamilisha usajili uliotajwa na kocha.
Credit:Anderson
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.