Staa wa Manchester United, Cristiano Ronaldo ametangaza kufiwa na mtoto wake wa kiume jioni ya leo Jumatatu Aprili 18, 2022 huku klabu yake ikielekea kumenyana na Liverpool mchezo wa ligi kuu nchini Uingereza.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram staa huyo amesema amefiwa na mtoto huyo wa kiume ambaye walikua mapacha pamoja na wa kike bila kufafanua ni huku akishukuru timu ya madaktari katika kujaribu kuokoa uhai wake mtoto huyo mchanga.
Ikumbukwe mwaka jana ilitangazwa kuwa mpenzi wa Mreno huyo, Georgina Rodriguez alikuwa mjamzito wa watoto pacha ambapo alitarajiwa kujifungua mwaka huu.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
“Kwa masikitiko makubwa tunatangaza kuwa mtoto wetu wa kiume amefariki dunia, ni maumivu makali ambayo mzazi yeyote anaweza kuyapata. Kuzaliwa kwa mtoto wetu wa kike ni Faraja kwetu kuendelea kuwa na furaha. Tunawashukuru madaktari na wauguzi wote kwa juhudi zao walizozifanya. Sote tuna huzuni kwa kumpoteza mpendwa wetu, kwa pamoja tunaomba suala hili libaki kuwa la familia wakati huu mgumu.
‘Mwanetu wa kiume, wewe ni Malaika, tutaendelea kukupenda.”Aliandika Ronaldo katika barua yake ya Mtandaoni.