Hatimaye baada ya sakata la muda mrefu la usajili wa mshambuliaji wa klabu ya Yanga sc Clement Mzize sasa mchezaji huyo kuna asilimia kubwa akaondoka nchini baada ya klabu ya Yanga sc kukubali kumuuza staa huyo kwa dau la dola milioni moja ambayo ni takribani kiasi cha shilingi bilioni 2.7 za kitanzania.
Awali kulikua na kizungumkuti kuhusu usajili wa mshambuliaji huyo huku malalamiko yakitawala hasa kutoka kwa meneja wa mchezaji huyo Bi Jasmine Razack ambaye alidai kuwa klabu ya Yanga sc ina roho mbaya baada ya viongozi wa klabu hiyo kukataa takribani dola laki sita kutoka klabu ya Al Masry ya nchini Misri ambayo ilishakubali kumlipa mchezaji huyo mshahara wa takribani dola elfu hamsini ambazo ni sawa na zaidi ya shilingi milioni mia moja za kitanzania.
“Niseme tu Yanga wana roho mbaya hawataki kumwachia Mchezaji, Al Masry wamekuja na ofa ila Yanga wamegoma wanataka dola Million moja kumwachia wakati Mayele tu aliondoka kwa dola 500,000 niseme tu Yanga wana roho mbaya na hawataki kumwachia wao wana hela hivyo wana kiburi, walikuwa wanamlipa Million mbili ila ndio mwaka huu wamemlipa Million 15 ila hawataki akachukue zaidi, naiomba Serikali watazame sana usimamizi wa mpira, wengi wanadidimiza na kuwaonea Wachezaji kisa hali duni”Alinukuriwa msimamizi wa mchezaji huyo Bi.Jasmini akizungumza na vyombo vya habari kuhusu kukwama kwa usajili wa mshambuliaji huyo.
Hata hivyo wakati meneja huyo akisema hivyo ilidaiwa kuwa Yanga sc walikua wamekubali kumuuza mshambuliaji huyo kuna klabu ya Al Sadd ambayo ilikua tayari kulipa kiasi cha takribani bilioni 2.7 kwa ajili ya kumsajili staa huyo lakini utata ulikua katika maslahi binafsi jambo ambalo kambi ya mchezaji huyo ilihitaji kiasi cha dola elfu hamsini kwa ajili ya kukubali mchezaji huyo kujiunga na klabu hiyo.
Hata hivyo wakati utata huo ukiendelea na kuzua mijadala katika vyombo vya habari hapa nchini,Mambo yameonyesha kubadilika baada ya klabu ya Esperance de Tunisia kukubali kulipa kiasi kinachohitajika na Yanga sc huku pia ikubali kumlipa mchezaji huyo mshahara mnono na marupurupu kibao ili ajiunge na klabu hiyo.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Kuja kwa dili kumeonyesha kukubalika kwa pande zote ambapo sasa dili hilo linaelekea kukamilika huku ikisaliwa na makubaliano madogo madogo ya kimkataba na baina ya pande hizo ambapo kwa sasa inatarajiwa kuwa mchezaji huyo akimaliza michuano ya mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (Chan) basi moja kwa moja ataondoka nchini na kujiunga na timu hiyo mpya.
Msimamo wa Yanga sc ulikua ni lazima staa huyo auzwe kwa bei hiyo huku pia msimamizi wa mchezaji huyo akiona kuwa dau hilo ni kubwa kwa thamani ya mchezaji huyo na ndio maana alikua anaona kama anakomolewa lakini sasa hali baina ya pande mbili inaelekea kutulia kwa faida kubwa ya mchezaji huyo.