Klabu ya Simba sc imefanikiwa kumuuza staa wake Pape Osmane Sakho kwenda klabu ya Quevilly Rouen Metropole (QRM) inayoshiriki ligi ya daraja la kwanza ya nchini Ufaransa.
Pape anaondoka Simba sc baada ya kukaa klabuni hapo kwa misimu miwili huku alikua amesaliwa na mkataba wa mwaka mmoja.
Katika dili hilo Simba sc imepata takribani dola laki sita huku pia kukiwa na mgawo kwa chama cha soka cha Senegal na klabu yake ya zamani ya Fc Teungueth FC ya nchini Senegal nayo ikipata mgawo katika dili hilo.
Kuondoka kwa mchezaji huyo hakukua na namna zaidi ya furaha kwa viongozi wa Simba sc kwani wamepata hela za kutosha huku pia wakiwa tayari wamemsajili Luis Miqqueson kwa ajili ya kuziba nafasi hiyo.