Home Makala Salamba Atemwa Js Soura

Salamba Atemwa Js Soura

by Sports Leo
0 comments

Mshambuliaji Mtanzania Adam Salamba ametemwa na klabu yake ya Js Soura ya nchini Algeria kutokana na kiwango kisichoridhisha baada ya kukaa klabuni hapo kwa muda wa miezi kumi tangu asajiliwe.

Awali mchezaji huyo alikwenda Uarabuni kusakata soka la kulipwa kisha kurudi nchini kutokana na changamoto za ugonjwa wa Covid 19 ambapo alijiunga na Namungo Fc ambapo hakudumu sana akapata dili la kujiunga na Js Soura.

Inasemekana kuwa benchi la ufundi la klabu hiyo halijaridhishwa na kiwango cha mchezaji huyo tangu ajiunge na klabu hiyo hivyo kufikia uamuzi wa kuachana nae.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited