Home Makala Samatta Kukatwa Mshahara

Samatta Kukatwa Mshahara

by Sports Leo
0 comments

Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania ,Mbwana Samatta anayecheza ndani ya Aston Villa ya England pamoja na wenzake watakatwa mshahara kwa asilimia 25 kwa miezi minne ili kuinusuru klabu yao kiuchumi wakati huu wa janga la Corona.

Wachezaji wa kikosi cha kwanza cha Aston Villa ,Makocha na Wasimamizi wakuu ndio watakaokatwa asilimia 25 ya mishahara yao kwa kipindi hiki cha Covid-19.

“Wachezaji wetu na wafanyakazi wana mshikamano mkubwa ,klabu nyingi za mpira wa miguu zina shida ya kifedha “alisema mtendaji mkuu wa Aston Villa ,Christian Purslow.

banner

Aliongeza kwa kusema kuwa wanaamini ni sahihi na ligi kuu inachukua hatua ya fedha zake ili kuwezesha kuendelea kutoa msaada muhimu wakati wote wa michezo England.

Awali Samatta ambaye pia anajilinda dhidi ya Covid 19 alikaririwa akisema ugonjwa huo unaweza kupangua malengo aliyojiwekea kwenye soka na kiuchumi kiujumla.

Aston Villa inashika nafasi ya 19 katika msimao wa ligi kuu ikiwa na pointi 25 baada ya kucheza mechi 28 pia ipo kwenye hatari ya kushuka daraja endapo itashindwa kupata ushindi katika mechi zilizobaki.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited