Home Makala Sasa Itakuwaje,Singida United?

Sasa Itakuwaje,Singida United?

by Sports Leo
0 comments

Kipa namba moja Singida United ambaye pia aliwahi kukipiga ndani ya Mbeya City ,Owen Chaima amesema kuwa hataweza kuwa na timu hiyo ligi daraja la kwanza kwa kuwa anaamini katika uwezo wake akiwa langoni.

Owen ambaye anakosa kujua hatima ya kesho yake ndani ya Singida United kutokana na kutokuwa na mkataba amejiweka sokoni kwa timu yoyote itakayo muhitaji hapa bongo na kuahidi kufanya makubwa zaidi.

“Nina uwezo mkubwa hilo lipo wazi kwani mashabiki wanajua kwamba nilikuwa Mbeya City na nilitoka na clean sheet nyingi tofauti na hapa Singida United mambo yamekuwa magumu kwani  mechi nyingine tulikuwa tunafungwa mabao mengi hiyo ilikuwa inatuumiza,hivyo nikipata timu nyingine hapa Bongo nitafanya makubwa zaidi” alisema Chaima.

banner

Kipa huyo alikaa langoni jana Julai 15, huku timu yake ikikubali kichapo cha mabao 3-1 mbele ya Yanga Uwanja wa Taifa.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited