Serikali imeongeza kiwango cha kodi kwa washindi wa michezo ya kubashiri (Betting) kwenye bajeti ya serikali kuu iliyosomwa jana bungeni ili kuongeza mapato kwa serikali.
Waziri wa Fedha Dkt.Mwigulu Nchemba amesema kuwa Ongezeko la kiwango hicho cha fedha kitakachopatikana, asilimia 70 itaenda katika mfuko wa serikali kupambana na Ukimwi na asilimia 30 kuchangia mfuko wa bima ya afya.
“Kufanya marekebisho kwenye sheria ya michezo ya kubahatisha sura namba 41. Kuongeza kiwango cha kodi kwenye zawadi ya ushindi kutoka asilimia 10 hadi asilimia 15,” amesema Waziri Mwigulu Nchemba bungeni Dodoma leo wakati akisoma bajeti ya mwaka wa fedha 2025/2026.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Tangu serikali iliruhusu michezo ya kubashiri nchini kuanzia mwaka 2015 ambapo imekua ikitunga sheria mbalimbali ili kuratibu michezo sambamba na kuhakikisha kuwa mapato yanapatikana kwa wingi.