Home Makala Shitshimbi Matatani,Ampiga Mwandishi

Shitshimbi Matatani,Ampiga Mwandishi

by Sports Leo
0 comments

Nahodha wa klabu ya Yanga Mkongomani Papy Kabamba TShishimbi ameingia matatani baada ya kumpiga mwandishi wa habari za michezo kwenye uwanja wa ndege jijini Dar es salaam jana wakati timu hiyo ikiwasili kutokea Mwanza.

Mwandishi huyo anayejulikana kama David Felician anayefanya kazi katika blogi ya Shaffihdauda.com ambayo inamilikiwa na mkuu wa vipindi wa Clouds Media Shaffih Dauda amepigwa na mchezaji huyo wakati akitimiza majukumu yake ambapo baada ya kumhoji kocha Mwinyi Zahera alienda kumhoji Shitshimbi ndipo akakutana na kipigo hicho.

Sportsleo bado linafatilia kujua chanzo hasa cha mchezaji huyo kumpiga mwandishi na hatua zaidi zilizochukuliwa na mwandishi huyo.

banner

Aidha tunatoa pole kwa mwandishi huyo pia tukiwaasa wachezaji kuwa michezo ni furaha na amani hivyo wote waandishi na wachezaji tunategemeana katika kutimiza majukumu ya kila siku.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited