Patrick Sibomana ambaye hapo awali alikuwa akiitumikia Yanga Sc amesaini dili la mwaka mmoja kuichezea klabu ya Polisi Rwanda ya Rwanda.
Sibomana mwenye umri wa miaka 25 alimaliza mkataba wake ndani ya Yanga Sc msimu uliopita na alifanikiwa kutupia jumla ya mabao sita ndani ya ligi kuu bara kati ya mabao 45.
Nyota huyo ametua Polisi Rwanda inayoshiriki ligi kuu ya nchini Rwanda japo awali tetesi zilikuwa zinaelezwa kuwa angetua ndani ya SC Kiyovu.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.