Home Makala Simba Day ni “Sold Out”

Simba Day ni “Sold Out”

by Sports Leo
0 comments

Mpaka sasa klabu ya Simba Sc imebakisha tiketi chache kuujaza uwanja wa Benjamin Mkapa ikiwa ni siku mbili kabla ya Tamasha la Simba Day kufanyika katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam ikiwa ni siku maalumu ya kutambulisha mastaa wa timu hiyo.

Mashabiki wa Simba Sc wameonekana kuhamasika zaidi na kununua tiketi kwa ajili ya tamasha hilo ambapo mpaka sasa zaidi ya mashabiki 52000 wakiwa tayari wameshanunua tiketi hizo kuelekea siku hiyo maalumu iliyoanzishwa na aliyekua mwenyekiti wa timu hiyo Mzee Hassan Dalali.

 

banner

Mapema klabu hiyo ilimaliza tiketi za majukwa makuu ya Platnum na V.I.P A na sasa leo tayari wamemaliza tiketi za mzunguko huku zikisalia tiketi zisizozidi 8000 katika majukwaa ya V.I.P B,C na machungwa ambazo mpaka kufikia siku ya ijumaa zitakua zimeisha kwa mujibu wa mwenendo wa tiketi mpaka sasa.

Simba sc hii haitakua mara ya kwanza kuujaza uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es salaam ikiwa huu ni utaratibu wao wa kawaida hasa katika michezo ya kimataifa ambapo mashabiki wa klabu hiyo hujitokeza kwa wingi kuingia viwanjani.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited