Home Makala Simba Kuivaa Ndanda Fc Leo

Simba Kuivaa Ndanda Fc Leo

by Sports Leo
0 comments

Kikosi cha Simba kipo tayari kuvaana na Ndanda Fc inayoshiriki ligi daraja la kwanza leo Octoba 13,katika uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi jijini Dar-es-salaam.

Mchezo huo utakaochezwa majira ya saa 11:00 jioni huku kiingilio kwa mzunguko ni buku saba (7,000) unawaandaa Simba ambao ni mabingwa watetezi wa ligi kuu bara kwenye mchezo wa raundi ya sita wa ligi dhidi ya Tanzania Prisons utakaochezwa Oktoba 22, Uwanja wa Nelson Mandela.

Ofisa habari wa Simba Sc,  Haji Manara amewaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi Azam Complex ili waje kuona burudani nzuri itakayowapatia matokeo chanza kutoka kwa wachezaji wao.

banner

“Hatuchezi tu ilimradi tunacheza bali tunacheza na kutoa burudani ,Simba ni timu ambayo inakupa burudani na kukupa matokeo, mashabiki mjitokeze kwa wingi kuipa sapoti timu,” alisema Manara.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited