Mabingwa watetezi Simba Sc imekamilisha raundi ya kwanza ya ligi kuu bara siku ya jana ambapo iliwapa kichapo Polisi Tanzania cha mabao 2-1 katika uwanja wa Benjamin Mkapa.
Polisi Tanzania walianza kujipatia bao la kwanza dakika ya 22 kupitia kwa Sixtus Sabilo huku bao la kusawazisha kutoka Simba lilipatikana kupitia John Bocco dakika ya 56 na ushindi ulikamilika pale ambapo Ibrahim Ajibu alichekelea nyavu dakika ya 90.
Simba Sc wanaongoza nafasi ya kwanza wakiwa na pointi 50 kwenye mechi 19 alizocheza huku Polisi Tanzania ikiwa nafasi ya saba na pointi 30 katika mechi ya 19.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.