Simba Sc imeanza safari yake leo Oktoba 19,kuelekea Mbeya kwa ajili ya mchezo wa raundi ya sita wa ligi kuu bara dhidi ya Tanzania Prisons.
Wanamsimbazi hao watakaa kwa muda wa siku mbili jijini Mbeya kabla ya kuelekea Rukwa kwa ajili ya mchezo huo utakaochezwa Oktoba 22, Uwanja wa Nelson Mandela majira ya saa 10:00.
Tanzania Prisons leo Octoba 19,watakuwa kibaruani kuchuana na JKT Tanzania uwanja wa Jamhuri Dodoma kwenye mchezo wa ligi kuu bara na baada ya hapo watarejea Rukwa kwa ajili ya kuvaana na Simba.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Simba Sc anbao ni mabingwa watetezi wa ligi kuu bara msimu uliopita ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 13 baada ya kucheza mechi tano msimu huu.