Simba Queens imeibuka na ushindi wa mabao 5 -0 mbele ya Baobab Queens leo kwenye mchezo wa Ligi ya Wanawake uliochezwa Uwanja wa Uhuru.
Ushindi huo unaifanya Simba Queens kutangazwa kuwa mabingwa wa Ligi ya Wanawake kwa kuwa wamefikisha jumla ya pointi 53 ambazo hazitaweza kufikiwa na timu yoyote kwa sasa ndani ya ligi hiyo.
Simba Queens wamebakiwa na mechi mbili za kucheza ambazo ni dhidi ya Alliance Girls na TSC Queens yote hiyo itakuwa kanda ya ziwa.