Klabu ya Wanawake ya Simba queens imeshindwa kufuzu hatua ya fainali ya kombe la wanawake barani Afrika baada ya kufungwa 1-0 na timu ya wanawake Mamelod Sundowns ya nchini Afrika ya kusini.
Simba queens inayoshiriki michuano hiyo kwa mara ya kwanza iliwashangaza wengi kutokana na kuonyesha kiwango bora katika michezo ya awali na kufanikiwa kufuzu hatua ya nusu fainali ambapo imekwaa kisiki hicho.
Kipindi cha kwanza kilimalizika kwa klabu hizo kwenda mapumziko ikiwa 0-0 lakini mambo yalibadilika kipindi cha pili dakika ya 75 baada ya shuti la Joyce Rabale kushinda kipa wa Simba queen na kujaa wavuni ambapo bao hilo lilidumu mpaka mwisho wa mchezo huo.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Wadada hao wa Mamelodi Sundowns walipiga jumla ya pasi 458 passes katika mchezo huo ikilinganishwa na pasi 266 zilizopigwa na Simba Queens.