Home Makala Simba Sc Bingwa Muungano Cup 2024

Simba Sc Bingwa Muungano Cup 2024

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Simba sc imefanikiwa kuibuka mabingwa wa kombe la Muungano baada ya kuifunga Azam Fc 1-0 katika mchezo wa fainali uliofanyika katika uwanja wa Amani Complex uliopo mjini Unguja Visiwani humo.

Pamoja na Azam Fc kushambulia mara kwa mara lakini ni Simba sc iliofanikiwa kupata bao dakika ya 77 ya mchezo likifungwa kwa kichwa na kiungo Babacar Sarr akiunganisha mpira wa faulo iliyopigwa na Mohamed Hussein kufuatia Willy Esomba Onana kuangushwa na Lusajo Mwaikenda.

Simba sc ilipaswa kuibuka na ushindi mnono lakini kukosa umakini kwa Fredy Michael kuliwatatiza ambapo alikosa mabao ya wazi sambamba na Onana aliyekosa nafasi kadhaa za dhahabu.

banner

Michuano ya Muungano imerejea rasmi mwaka huu baada ya kusimama kwa miaka mingi ambapo zamani michuano hiyo ilikua ni yenye msisimuka wa hali ya juu na mwaka huu umeshirikisha timu nne za Simba sc na Azam Fc kutoka Tanzania bara huku Kmkm na Kvz kutoka Visiwani Zanzibar.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited