Baada ya kufanikiwa kuchukua alama tatu katika mchezo wa pili wa ligi kuu dhidi ya Dodoma Jiji Fc klabu ya Simba sc sasa imefanikiwa kukaa kileleni mwa ligi kuu ya soka ya Nbc nchini.
Simba sc iliibuka na ushindi wa mabao mawili katika mchezo huo uliochezwa katika uwanja wa uhuru jijini Dar es salaam mabao yakifungwa na Jean Baleke dakika ya 43 na Moses Phiri dakika ya 55 na kupeleka furaha kwa mashabiki wa klabu hiyo ambao hawakujitokeza kwa wingi kama ilivyo kawaida yao.
Safu ya ulinzi ya Simba sc pamoja na kufanya vibaya dhidi ya Mtibwa Sugar na kuruhusu mabao mawili jana ilifanya vizuri ikiwa chini ya Che Malone Fondoh na Kennedy Juma huku pembeni wakicheza Shomari Kapombe na Mohamed Hussein na eneo la kiungo walitawala Mzamiru Yassin na Fabrice Ngoma.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Sasa Simba sc kutokana na ushindi huo imefikisha alama sita kileleni mwa msimamo huku ikiwa jumla imefunga mabao sita katika ligi kuu na kufungwa mabao mawili.