Home Makala Simba sc Kuwavaa Power Dynamos

Simba sc Kuwavaa Power Dynamos

by Sports Leo
0 comments

Katika kilele cha siku ya Simba day ambayo mwaka huu itafanyika agosti 6 katika uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es salaam klabu ya Simba sc imewaalika timu ya PowerDynamos ambao ni mabingwa wa ligi kuu ya soka nchini Zambia msimu uliopita.

Tamasha hilo kubwa maalumu kabisa kwa ajili ya kutambulisha wachezaji wapya kwa mashabiki wa klabu hiyo litatumia kauli mbiu ya “UNYAMA MWINGI” kwa mwaka huu na uzinduzi wake utafanyika mapema Julai 29 maeneo ya Buza na kilele kitakua Agosti 8 mwaka huu huku kukiwa na matukio kama yafuatay0.

▪️Kuchangia damu
▪️Usafi -sehemu mbali mbali ulipo
▪️Kuchagia wodi ya mama na mtoto
▪️Kuchangia Wodi ya Hospital zanzibar
▪️Siku maalumu ya kuwatembelea mashujaa (legends waliopita Simba)
▪️Siku ya Kuwatembelea wazee wa Simba Sc
▪️Uzinduzi wa matawi ya Simba (Buza Kanisani)

banner

Kwa mujibu wa Meneja habari wa klabu hiyo kikosi cha timu hiyo kinatarajiwa kurejea nchini kuanzia Agosti mosi tayari kabisa kwa kushiriki matukio mbalimbali ya wiki hiyo.

 

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited