Mchana wa leo droo ya Ligi ya Mabingwa Afrika imepangwa ambapo Simba sc itaanzia Raundi ya Pili kwa kucheza na mshindi wa mechi kati ya Power Dynamos (Zambia) dhidi ya African Stars (Namibia).
Simba sc itaanzia raundi ya pili tofauti na watani zao Yanga sc kutokana kufanya vizri zaidi katika miaka mitano iliyopita ambapo wamepatia alama nyingi kiasi cha kuwa katika nafasi ya tisa kwa ubora katika ngazi ya vilabu barani Afrika.
Endapo Simba sc itapata matokeo katika michezo hiyo miwili ambayo itaanzia ugenini na kumalizia nyumbani basi moja kwa moja itakua imefuzu hatua ya makundi barani Afrika.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Timu hizo za Power Dynamos na African Stars hazionekani kuwa tishio mbele ya Simba sc kutokana na aina ya usajili waliofanya msimu huu pamoja na nafasi yao katika soka la Afrika.