Home Makala Simba sc Mwendo wa 5G

Simba sc Mwendo wa 5G

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Simba sc imeibuka na ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa ligi kuu nchini uliofanyika katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam na kufanikiwa kupanda mpaka nafasi ya pili ya msimamo wa ligi kuu nchini.

Ikifaidika na kurejea kwa Shomari Kapombe aliyekua majeruhi na Mzamiru Yassin aliyemaliza adhabu ya kadi tatu za njano,Simba sc ilipata bao la uongozi dakika ya 38 ya mchezo likifungwa na Mazimiru kwa shuti kali baada ya kupokea pasi ya Augustine Okrah huku dakika chache baada ya kipindi cha pili kuanza Pape Sakho alifunga goli la pili kwa Simba sc na ikiwa la pili kwake katika ligi kuu nchini msimu huu.

Dakika ya 63 Okrah alifunga bao la tatu na dakika 10 baadae Phiri alifunga la nne kwa shuti kali huku kalamu ya mabao ikimaliziwa na Sakho aliyefunga bao la tano kwa kichwa kikali na kuzua furaha kwa mashabiki wa klabu ya Simba sc.

banner

Katika mchezo Mtibwa walipata majanga baada ya kipa Faroukh Shikhalo kuumia huku kiungo Kitenge na beki Cassian Ponera wakipata kadi nyekundu.

Simba sc sasa imerejea katika nafasi ya pili ya msimamo ikifikisha alama 17 nyuma ya Yanga sc ambao nao wamecheza michezo nane ya ligi kuu nchini.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited