Klabu ya Simba imepangwa kucheza na klabu ya Al-Ahly kwenye michuano ya African football league inayotarajiwa kufunguliwa hapa nchini siku ya 20 Oct 2023 katika uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es salaam.
Mshindi katika mchezo huo atakutana na mshindi baina ya Petro De Luanda ya nchini Angola dhidi ya Mamelodi Sundowns ya Africa ya kusini a,bapo michuano hiyo inatarajiwa kuanzia hatua ya robo fainali huku ikishirikisha timu nane bora barani Afrika.
Simba sc inatarjiwa kupata upinzani mkali katika mchezo huo ikizingatiwa kiwango cha Al ahly katika michuano ya kimataifa huwa kiko juu huku wakiwana uzoefu wa kutosha kucheza hatua za mtoano hasa wakiwa wanaanzia ugenini na kumalizia nyumbani.
Ili ifuzu kwenda nusu fainali Simba sc haina budi kushinda mabao mengi hapa nyumbani kitu ambacho ni kigumu ikizingatiwa kuwa Al Ahly ina wachezaji wa viwango vya juu hasa Percy Tau ambaye alisajiliwa kutokea katika ligi kuu ya nchini Uingereza.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.