Zikiwa zimesalia siku kadhaa kabla ya kurejea nchini klabu ya Simba sc imetangaza kuwa itacheza michezo miwili ya kirafiki ikiwa katika kambi ya maandalizi ya kumalizia awamu ya pili ya msimu wa ligi kuu pamoja na michuano ya kimataifa iliyoko Dubai nchi za falme za kiarabu.
Simba sc iliondoka nchini wiki iliyopita baada ya kutolewa katika michuano ya kombe la Mapinduzi ambapo kikosi hicho pamoja na kocha mpya Roberto Oliveira walipewa ofa hiyo ya kambi ili kocha huyo aweze kukaa na kikosi katika mazingira tulivu ili kuingiza mbinu zake kwa mastaa hao.
Simba sc kupitia mitandao yake ya kijamii imetangaza kucheza michezo miwili ya kirafiki katika kujaribu mbinu za kocha huyo ambapo timu hiyo itavaana na CSKA Moscow ya Urusi ambao ni mabingwa wa ligi ya klabu bingwa barani ulaya mwaka 2005 ambapo mchezo huo utafanyika Januari 15 huku mchezo mwingine dhidi ya timu ya Al Dhafra ukufanyika Januari 13.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Baada ya michezo hiyo Simba sc itarejea haraka nchini kuja kuvaana na Mbeya city siku ya Jumanne januari 17 jijini Dar es salaam katika uwanja wa Benjamin Mkapa.