Home Soka Simba Sc Wanasa Kiungo wa Mali

Simba Sc Wanasa Kiungo wa Mali

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Simba sc ipo mbioni kumsajii kiungo wa klabu ya Red Arrows ya Zambia mwenye uraia wa Mali Allasane Diarra ambaye anakuja kuwasaidia Cletous Chama na Rally Bwallya ambaye yupo mbioni kukamilisha dili la kujiunga na klabu ya Amazulu Fc ya nchini Afrika kusini.

Usajili wa kiungo huyo ni moja ya mapendekez0 ya benchi la ufundi lililotimuliwa chini ya Pablo Franco ambaye alikubaliana na uongozi wa klabu hiyo kabla hajatimuliwa hivyo uongozi wa klabu hiyo ulianza kulifanyia kazi suala hilo na kufanikiwa kumnasa Kiungo huyo baada ya kuwakosa Victorien Adebayo na Aziz Ki ambaye ananyemelewa pia na Yanga sc.

Simba sc imevutiwa na Diarra ambaye aamewakosha mabosi wa Simba sc kutokana na kiwango chake bora alichoonyesha kwenye ligi yao, Kombe la Shirikisho ikiwemo mechi mbili dhidi ya Simba ambazo zote alianza.

banner

“Unajua tumekubaliana kwenye kila nafasi moja tuliyopanga kusajili mchezaji mpya wa kigeni tumeweka chaguo la kwanza hadi la nne kulingana na viwango vyao vilivyo,” alisema bosi mmoja ndani ya Simba na kuongeza;

“Tumeamua kufanya hivyo ili kuweka nguvu kusajili mchezaji chaguo la kwanza kama tukishindwa tunashuka chini kwa maana chaguo la pili, tatu au nne na naamini tutafanikisha kumpata mmoja kati yao.”Kilisema chanzo chetu cha habari kutoka klabuni Simba sc.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited