Home Makala Simba Sc Yaachana na Okrah

Simba Sc Yaachana na Okrah

by Dennis Msotwa
0 comments

Sasa rasmi klabu ya Simba sc imetangaza kuachana na winga Augustine Okrah baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa msimu mmoja pekee huku majeraha ya mara kwa mara pamoja na matatizo ya utovu wa nidhamu ya mara kwa mara.

Simba sc ilimsajili Okrah kutoka Benchem United inayoshiriki ligi kuu nchini Ghana ambapo staa huyo alikua na takwimu bora kabisa zilizowavutia Simba sc akifunga mabao 14 katika mechi 32 za ligi kuu nchini humo.

Taarifa za kuachwa kwa Okrah zimetangazwa katika vyanzo rasmi vya klabu vya mitandao ya kijamii ya klabu hiyo na kumaliza tetesi za muda mrefu za kutemwa kwa staa huyo ambaye wapenzi wengi wa klabu hiyo walikua na matarajio makubwa na staa hiyo

banner

“Baada ya kuwa kwenye kikosi chetu kwa msimu mmoja, Augustine Okrah hatakuwa sehemu ya timu yetu ya msimu ujao”ilisomeka taarifa kutoka katika mtandao wa kijamii wa facebook wa klabu hiyo.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited