Klabu ya Simba sc imeendeleza dozi ya mabao kwa timu ya Cosmopolitan Fc baada ya kuibamiza kwa mabao 5-1 katika mchezo wa kujipima nguvu ikijiandaa na michuano ya kimataifa hasa hatua ya pili ya michuano ya klabu bingwa barani Afrika na michuano mipya ya ligi inayojumuisha timu nane bora barani Afrika.
Juzi Simba sc iliibamiza Kipanga Fc kwa idadi ya mabao 3-0 yakifungwa na Moses Phiri,Aubin Kramo na Luis Miquissone na leo mapema imeibuka na ushindi huo kwa mabao ya Moses Phiri,Jean Baleke,Leandre Onana,Aubin Kramo na Shaban Idd Chilunda.
Simba sc itavaana na Power Dynamos ya Zambia katika mchezowa kuwania kufuzu hatua ya makundi ya klabu bingwa Septemba 17 nchini Zambia ambapo timu hizo zitarudiana nchini baada ya wiki mbili.
Licha ya kuanza mdogomdogo kutafuta utimamu wa mwili baadhi ya mastaa wa Simba sc wameanza kuimarika hasa Luis Miqquisone ambaye usajili wake ulivuma sana hapa nchini kiasi cha wengi kumfuatilia zaidi.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
“Jambo zuri ni baadhi ya wachezaji wetu kuanza kuimarika hasa Luis ambaye. ni mchezaji mkubwa na anajua kuamua mechi kama hizi sasa amepungua uzito anarudi kwenye kiwango chake huku pia Inonga amerejea na sasa tunasubiri kusikia kuhusu Aishi”Alisema kocha wa klabu hiyo Roberto Oliveira maarufu kama Robertinho wakati akiongea na mwandishi wetu.