Home Makala Simba sc Yafuzu Kibabe Caf

Simba sc Yafuzu Kibabe Caf

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Simba sc imefanikiwa kufuzu hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa barani Afrika ikiifunga klabu ya Premero De Augosto ya Angola kwa ujumla ya ushindi wa jumla wa mabao 4-1 baada ya jana kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 1-0 katika mchezo wa pili uliofanyika katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Awali katika mchezo wa awamu ya kwanza nchini Angola uliofanyika katika uwanja wa Novemba 11 Simba sc ilipata ushindi wa mabao 3-1 kutokana na mabao ya Cletous Chama,Israel Mwenda na Moses Phiri na kurahisisha kazi katika mchezo wa marudiano uliofanyika hapa nyumbani hapo jana ambapo ilipata ushindi wa 1-0.

Katika mchezo huo ambao mashabiki wa klabu hiyo walifurika vya kutosha Simba sc ilifanikiwa kuandika bao dakika ya 33 kupitia kwa Moses Phiri aliyepokea pasi ya Mohamed Hussein na kuandika bao hilo pekee katika mchezo huo na mpaka mpira unamalizika ubao wa matokeo ulisoma 1-0.

banner

Simba sc sasa imefanikiwa kuungana na miamba ya soka mbalimbali barani Afrika katika kucheza hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa barani Afrika ambapo sasa itasubiri droo ya kupanga makundi huku ikipaswa kujiandaa kuvaana na timu kubwa na zenye uwekezaji mkubwa barani Afrika kama vile Al Ahly,Al Hilal Fc na wengineo.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited