Home Makala Simba sc Yafuzu Makundi Caf

Simba sc Yafuzu Makundi Caf

by Dennis Msotwa
0 comments

Klabu ya Simba sc licha ya kupata sare ya 1-1 na Power Dynamos ya Zambia katika mchezo wa ligi ya mabingwa barani Afrika uliofanyika katika uwanja wa Azam Complex Chamazi jumapili Oktoba 1 2023.

Katika mchezo wa awali nchini Zambia timu hizo zilitoa sare ya 2-2 na kufanya kusubiri mchezo wa marudiano nchini kuamua nani anafuzu makundi msimu huu.

Dynamos iliwashangaza mashabiki wa Simba sc kwa bao la mapema dakika ya 16 na Andy Boyeli kwa shuti kali lililomshinda kipa Ayoub Lakred na kuzama wavuni huku mabeki wa Simba sc wakibaki kulaumiana kutokana na kushindwa kuokoa mpira huo.

banner

Licha ya kupata goli hilo bado Dynamos waliendelea kulitawala eneo la katikati mwa uwanja na kufanikiwa kufika golini mwa Simba sc mara nyingi zaidi.

Bao la kujifunga la Kondwani Chiboni lilipeleka furaha msimbazi kwani ndio limekua tumaini pekee la timu hiyo kufuzu kwa goli la ugenini baada ya dakika tisini za mchezo.

Kwa mara ya kwanza Tanzania inaingiza timu mbili hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika kutokana na timu kongwe zaidi nchini za Simba sc na Yanga sc kufuzu msimu huu.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited