Home Makala Simba sc Yaifuata Tripoli

Simba sc Yaifuata Tripoli

by Sports Leo
0 comments

Msafara wa kikosi cha timu ya Simba Sc mapema kimeanza safari ya kuelekea nchini Libya tayari kwa mchezo wa hatua ya pili michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya Al Ahly Tripoli ya nchini humo.

Msafara wa mastaa wa timu hiyo umeondoka mapema ya leo na tayari umewasili salama nchini Uturuki ambapo watalala hapo usiku wa leo na mapema kesho watakwea pipa kuelekea nchini Libya.

Baadhi ya mastaa waliokua na timu zao za Taifa wakiwemo Mohammed Hussein,Edwin Balua na Ally Salim wenyewe wameanza safari tangu jana kuelekea nchini humo na wataungana na kikosi moja kwa moja nchini Libya.

banner

Simba sc na Tripoli wanatarajiwa kuumana siku ya Jumapili katika mchezo wa kwanza na watarudiana baada ya wiki moja na mshindi atafuzu moja kwa moja hatua ya makundi ya kombe hilo.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited