Home Makala Simba Sc Yaipiga Malindi Fc

Simba Sc Yaipiga Malindi Fc

by Dennis Msotwa
0 comments

Klabu ya Simba sc imefanikiwa kuibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Malindi Fc katika mchezo wa kirafiki uliofanyika katika uwanja wa Amani mjini Unguja bao la Nassoro Kapama ambaye alifunga kwa kichwa kufuatia kona safi ya Pape Osmane Sakho dakika ya 13 ya mchezo na mpaka filimbi ya mwisho inapigwa matokeo yalibaki hivyo hivyo.

Simba sc iliyoanza na wachezaji wengi ambao hawapati nafasi mara kwa mara kikosini akiwemo golikipa Ally Salim,Dejan,Nassoro Kapama na Nelson Okwa pamoja na Peter Banda ambao walikua hawajachanganya na kusababisha mpira kuwa wa kawaida huku Malindi wakionyesha ushindani wa hali ya juu.

Mechi hiyo ni muendelezo wa maandalizi ya kujiandaa na raundi wa pili ya michuano ya kimataifa ambapo Simba sc itawavaa De Augosto kutoka Angola baada ya kufanikiwa kuwafunga Nyassa Big Bullets katika michezo yote miwili nyumbani na ugenini.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited