Home Makala Simba sc Yamgomea Winga Mkenya

Simba sc Yamgomea Winga Mkenya

by Sports Leo
0 comments

Kejeli za mashabiki mitandao na kugawanyika kwa viongozi wa klabu Simba sc juu ya usajili wa winga Harrison Mwendwa ndio kumesababisha mchezaji huyo arudi nyumbani kwao Kenya bila kusaini Mkataba klabuni hapo licha ya kufanya mazungumzo na viongozi wa klabu hiyo.

Winga huyo aliwasili nchini wiki iliyopita kufanya mazungumzo ya mwisho pamoja na kusaini mkataba na klabu ya Simba sc lakini baadhi ya mabosi wa klabu hiyo hawakukubaliana kuhusu kumsaini mchezaji huyo kwa sababu tulizozitaha hapo juu lakini pia wengine wakiweka hoja ya kiwango cha mchezaji huyo kutokua sawa kama ilivyokua miaka miwili iliyopita ambapo klabu hiyo pia ilionyesha nia ya kumsajili.

Mwendwa winga wa zamani wa Mathare United, Kariobangi Sharks na AFC Leopards za nchini Kenya sasa tayari amerejea nchini kwao ambapo inasemekana anasikilizia ofa ya Singida Big Boys na ofa kutoka nchini Afrika ya Kusini ambapo kuna timu zimeonyesha nia ya kumsajili.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited