Home Soka Simba Sc Yamsajili Mpanzu

Simba Sc Yamsajili Mpanzu

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Simba Sc imekamilisha usajili wa kiungo mshambuliaji Ellie Mpanzu kwa mkataba wa miaka miwili pamoja na kipengele cha kuongeza mwaka mmoja zaidi kutokana na kuonyesha uwezo mzuri.

Mpanzu amesajiliwa kama mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba katika klabu ya As Vita ya nchini Dr Congo ambapo aliitumikia klabu hiyo kwa mafanikio makubwa.

Inasemekana zaidi ya shilingi milioni mia saba zimetumika kukamilisha usajili huo ambapo baadhi ya pesa amechukua mchezaji sambamba na mtu anayemmiliki mchezaji huyo kama ambavyo huwa kwa wachezaji wengi wa nchini humo kumilikiwa na watu binafsi.

banner

Mpanzu anatarajiwa kuanza kuitumikia Simba sc kuanzia mwezi disemba wakati wa usajili wa dirisha dogo utakapofunguliwa na anatarajiwa kuanza pia kutumika katika hatua ya makundi ya kombe la Shirikisho barani Afrika.

Simba sc imeanza kuongeza nguvu kikosi chake baada ya kufanikiwa kufuzu hatua ya makundi ya kombe la Shirikisho barani Afrika ikiwafunga Al ahly Tripol ya Libya kwa mabao 3-1 katika mchezo wa marudiano wa hatua ya pili ya michuano hiyo uliofanyika katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Pamoja na Mpanzu pia mabosi wa klabu hiyo wanaangalia uwezekano wa kumsajili Feisal Salum kutoka Azam Fc kuongeza nguvu kikosi hicho kwa ajili ya ligi kuu na michuano ya Kimataifa.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited