Klabu ya Simba Sc imefanikiwa kukamilisha usajili na kumtambulisha beki Rushine De Reuck kutoka klabu ya Mamelodi Sundowns kwa mkopo wa mwaka mmoja akichukua nafasi ya Che Malone Fondoh ambaye amepata timu Uarabuni.
Rushine anasifika kwa kucheza kama beki wa kati ama kulia pamoja na kiungo mkabaji akiwa majukumu ya kiulinzi zaidi.
Simba sc imekamilisha usajili huo ili kuipa nguvu zaidi safu ya ulinzi ya klabu hiyo ambayo haijachukua ubingwa wa ligi kuu kwa miaka minne sasa.
Tajiri wa klabu ya Simba Sc Mohammed Dewji msimu huu ameahidi kufanya usajili mkubwa wa kishindo ili kurudisha furaha kwa mashabiki wa klabu hiyo.
Kocha Fadlu Davis ndie yupo mstari wa mbele zaidi msimu huu katika kufanya usajili wa mastaa mbalimbali akiwa na nguvu ya kuamua nani wa kumsajili msimu huu.