Mastaa wa klabu ya Simba sc jioni ya leo wamepaa kwa ndege ya shirika la Emirates kuelekea nchini Dubai kwa ajili ya kambi ya siku kumi kujiandaa ni michuano ya kimataifa pamoja na ligi kuu nchini.
Kikosi hiko kimepaa baada ya kutolewa katika michuano ya kombe la Mapinduzi ambapo lengo kuu la ziara hiyo ni kumpa nafasi kocha mpya Robertinho aliyejiunga na timu hizo wiki hii akitokea Vipers Fc kujuana kwa undani zaidi na wachezaji ili asipate shida katika kupanga kikosi katika mechi.
Mastaa wa kikosi hicho karibia wote wamesafiri kutokea hapa nchini huku wachache wakitarajia kuungana na kikosi kutokea makwao walipokua wameenda kwa mapumziko mafupi.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.