Home Makala Simba sc Yapiga 7-0

Simba sc Yapiga 7-0

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Simba sc imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 7-0 dhidi ya Ruvu Shooting katika mchezo wa kombe la shirikisho uliofanyika katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Iliwachukua wekundu wa msimbazi dakika 2 kupata bao la uongozi kupitia kwa nahodha John Bocco aliyefunga pia bao la pili dakika ya 40 huku Cletous Chama akifanikiwa kufunga mabao matatu {Hattrick}  dakika za 23,25 na 73 huku dakika moja kabla ya mapumziko beki wa Ruvu Shooting Masinda alijifunga huku Jimson Mwinuke akifunga bao la saba na la mwisho dakika ya 70.

Simba sc imeweka rekodi ya kufunga mabao 13 katika michezo miwili inayifuatana ya kombe la shirikisho ikiwafunga Dar city 6-0 katika hatua ya 32 bora na ushindi wa 7-0 dhidi ya Ruvu Shooting hatua ya 16 bora huku ikiungana na Yanga sc,Azam Fc,Polisi Tanzania,Coastal Union,Kagera Sugar na Pamba Fc ya ligi daraja la kwanza.

banner

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited