Home Makala Simba Sc Yashusha Mzungu

Simba Sc Yashusha Mzungu

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya soka ya Simba sc imeamuajiri Mels Daalder kuwa skauti mkuu wa timu kwa ajili ya kutafuta vipaji vya wachezaji ambao watasajiliwa na klabu hiyo kwa ajili ya mashindano mbalimbali ya ligi kuu na ya kimataifa ambayo timu hiyo inatarajiwa kushiriki hasa msimu ujao.

“ Tunafuraha kubwa kumkaribisha Mels ili kuja kuboresha ufanisi kwenye scouting kwani ni eneo muhimu sana kwenye mafanikio ya klabu yetu. Tunaendelea na maboresho muhimu kuelekea msimu mpya wa ligi na mashindano ya kimataifa, ”Alisema Afisa mtendaji mkuu wa klabu hiyo Iman Kajula

Mels ambae ni raia wa Uholanzi ana uzoefu wa kufanya skaunti duniani ameshiriki kozi mbalimbali za kazi hiyo ikiwa ni pamoja na zile zilizoendeshwa na mkuu wa skaunti wa zamani wa Manchester United, David Hobson.

banner

Mels ambaye ni shabiki mkubwa wa Simba na pia ni mjuzi wa kufanya uchambuzi (soccer analysis) na ana ujuzi mkubwa wa ligi ya Tanzania, Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited