Katika michezo ya ligi kuu bara inayoendelea Simba wamefanikiwa kurudisha heshima baada ya kuwafunga Mbao Fc mabao 2-1 katika uwanja wao wa nyumbani CCM Kirumba jijini Mwanza.
Hassan Dilunga anakuwa wa kwanza katika kipindi cha kwanza kuipatia Simba bao moja dakika ya 41 kwa kupeleka mashambulizi katika lango la Mbao kwa guu la kushoto lililomshinda mlinda mlango wa Mbao.
Kipindi cha pili Jonas Mkude anaongeza bao la pili kwa Simba dakika ya 46 huku bao la kufutia machozi kwa Mbao walio chini ya Hemedi Moroco lilifungwa na Waziri Jr dakika ya 52.
Simba Sc wanafikisha jumla ya pointi 38 ikiwa nafasi ya kwanza katika mechi ya 13 ikiwaacha wapinzani wake Yanga kwa pointi 13 na ikiwa na michezo miwili ili kuwa sawa na Simba.