Home Makala Simba Yashusha Wabrazil

Simba Yashusha Wabrazil

by Sports Leo
0 comments

Simba kumenoga ndio msemo ambao unatamba kijiweni hivi sasa baada ya mabosi wa klabu hiyo kuamua kushusha mziki kamili baada ya kumaliza kuwasainisha mastaa waliomaliza mikataba yao ndani ya klabu hiyo akiwemo ”Bull striker” Meddie Kagere.

Basi baada ya kumaliza usajili huo sasa klabu hiyo imegeukia usajili wa wachezaji wapya na moja kwa moja wamemshusha beki wa kibrazil anayecheza pia kiungo mkabaji Gerson Fraga Vieira mwenye miaka 26 mzaliwa wa Porto Allegre nchini humo.

Mchezaji huyo hivi sasa ni mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake na timu ya Atletico de Kolkata(ATK) ya india mkataba ambao uliisha rasmi mwenye mei mwaka huu.

banner

Beki huyo mrefu utotoni aliichezea akademi ya Timu ya Gremio ya Brazil ambayo ni maarufu kwa kukuza mastaa kibao wa soka nchini humo akiwemo Ronadinho Gaucho,Douglas Costa wa Juventus na Staa wa sasa wa Barcelona Arthur Melo.

Takwimu zinaonyesha kuwa beki huyo licha ya kucheza nchini kwao pia amecheza kwa muda  mrefu nchini India na ameichezea Timu yake ya ATK mechi 21 na kufunga goli moja kwa msimu ulioisha.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited