Home Makala Singida Bss Kuishtaki Gormahia Fc

Singida Bss Kuishtaki Gormahia Fc

by Sports Leo
0 comments

Klabu ya Singida Black Stars ina mpango wa kuipeleka klabu ya Gor Mahia kwenye shirikisho la soka Duniani (FIFA) baada ya klabu hiyo kutorudisha fedha za usajili licha dili la nyota wake Ronney Onyango kujiunga na klabu hiyo kushindikana.

Singida Black Stars inaidai Gor Mahia kiasi cha USD 40,000 (TZS 101 Million) pesa ambayo waliilipa klabu hiyo kwaajili ya nyota huyo lakini nyota huyo aligoma kusaini mkataba na Black Stars.

Singida Black Stars walifuata taratibu zote za usajili ambapo walilipa mpaka kiasi walichokubaliana ili kukamilisha usajili huo lakini dili hilo lilikufa mwishoni baada ya staa huyo kugoma kuja nchini kusaini mkataba na klabu hiyo.

banner

Baada ya dili hilo kufa mabosi wa Singida Black Stars walijitahidi kuwasiliana na Gormahia Fc kurejesha kiasi hicho cha fedha lakini mpaka leo haijarudi.

Tayari Singida Black Stars imeanza harakati za kwenda kushtaki Fifa ili kupata suluhisho la fedha hizo ambapo endapo baada ya uchunguzi itabainika ni kweli basi Gormahia Fc watafungiwa kufanya usajili wa wachezaji wa ndani na nje ya nchi mpaka watakapo kamilisha malipo hayo.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited