Home Makala Skudu Is Back

Skudu Is Back

by Sports Leo
0 comments

Winga wa klabu ya Yanga sc raia wa Afrika kusini Mahlatse Makudubela ameendelea kufanya mazoezi ya pamoja na wachezaji wenzake walio salia kambini baada ya wengine kuelekea kwenye majukumu ya timu zao za Taifa baada ya kufanikiwa kupona majeraha yake.

Skudu aliumia katika mchezo wa ngao ya jamii baina ya Yanga sc dhidi ya Azam Fc uliofanyika katika uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga ambapo alicheza takribani dakika saba pekee na kulazimika kutolewa nje kwa matibabu zaidi ambapo alikaa nje kwa takribani wiki mbili.

Sasa baada ya kurejea nchini kutokea Afrika ya Kusini alipokwenda kwa ajili ya kuhuisha hati yake ya kusafiria staa huyo amerejea na kujiunga katika mazoezi ya timu yake mapema leo baada ya kumaliza mazoezi ya kuweka mwili sawa kutokana na majeraha,

banner

Skudu amekua mchezaji anayetegemewa na mashabiki wa klabu hiyo kuleta burudani baada ya kusajili klabuni hapo na kupewa jezi namba sita iliyokua ikivaliwa na Feisal Salum.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited