Home Makala Staa Yanga Sc Atua Fountain Gate Fc

Staa Yanga Sc Atua Fountain Gate Fc

by Sports Leo
0 comments

Imefahamika kuwa aliyekua mchezaji wa zamani wa klabu ya Yanga sc Yusuph Athuman amejiunga na klabu ya Fountain Gate Fc yenye makazi yake Babati mkoani Manyara.

Staa huyo ambaye sasa yuko zake jijini Dar es Salaam akijiandaa kujiunga na timu yake hiyo mpya wakati wa usajili wa dirisha dogo linatakalo funguliwa mwezi disemba.

Fountain Gate Fc imemsajili Athuman akiwa mchezaji huru ambapo ataungana na washambuliaji Edger William na Selemani Mwalimu Gomez kuunda safu ya ushambuliaji ya klabu hiyo kuanzia mwezi ujao.

banner

Yusuph anatarajiwa kuonyesha uwezo mkubwa kutokana na kuwa na kipaji bora alichokionyesha tangu akiwa Biashara United kisha Yanga Sc ambapo hakuonyesha kiwango kutokana na majeraha ya mara kwa mara.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited