Home Makala Stars Yapigwa Kufuzu Chan

Stars Yapigwa Kufuzu Chan

by Sports Leo
0 comments

Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imepoteza mchezo wa kuwania kufuzu michuano ya mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (Chan) baada ya kukubali kipigo cha 1-0 kutoka kwa Uganda katika mchezo uliofanyika katika uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es salaam.

Stars ilijitahidi kucheza kwa kupanga mashambulizi ya uhakika lakini uimara wa safu ya ulinzi ya Uganda ukawa kikwazo kupata bao hali iliyodumu mpaka mapumziko ya kipindi cha kwanza bila kupata bao.

Zikiwa zimesalia dakika tatu mchezo kukamilika, Uganda waliweza kupachika bao kupitia kwa Travis Mutyaba dakika ya 87 katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa bao ambalo lilianzia upande wa kushoto baada ya Mohamed Hussein kushindwa kuokoa mpira na kumkuta mfungaji.

banner

Kutokana na matokeo hayo Taifa Stars inakabiliwa na mtihani mzito wa kusaka ushindi wakati wa mchezo wa marudiano nchini Uganda  ambapo haitakua na matokeo mengine yenye nafuu zaidi ya ushindi wa kuanzia mabao mawili huku wakihakikisha wenyeji hawapati bao.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited