Home Makala Stars Yawasili Morocco Kukipiga J5

Stars Yawasili Morocco Kukipiga J5

by Sports Leo
0 comments

Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imewasili salama nchini Morocco ambapo inatarajiwa kucheza siku ya jumatano na timu ya Taifa hilo kuwania kufuzu fainali za kombe la Dunia mwaka 2026.

Stars inatarajiwa kucheza mchezo huo wa kundi E la kufuzu michuano hiyo ambapo italazimika kupambana kwa jasho na damu ili kuchukua alama tatu.

Mastaa mbalimbali wa Taifa Stars waliwasili katika uwanja wa ndege wa mfalme Mohammed wa VI tayari kwa kuliwakilisha Taifa katika mchezo huo.

banner

Mastaa wengine kama Selemani Mwalimu Gomez yeye amejiunga na timu hiyo moja kwa moja nchini humo kutokana na kuwa anaishi tayari huko akiichezea klabu ya Wydad Athletic.

Michuano ya kombe la Dunia kwa mwaka 2026 inatarajiwa kufanyika katika nchi za Marekani,Mexico na Canada ambapo mchezo wa fainali utakaofanyika katika jiji la Newyork nchini Marekani.

Katika msimamo wa kundi A Morocco anaongoza akiwa na alama 12 katika michezo minne huku Tanzania tukiwa katika nafasi ya tatu ya msimamo na alama 6 katika michezo mitatu.

You may also like

Leave a Comment

Sportsleo Bongo ni tovuti ya kwanza na bora zaidi ya michezo nchini Tanzania, ikileta habari kwa Kiswahili, matokeo ya moja kwa moja, tetesi, na taarifa muhimu kuhusu soka, ndondi, riadha na michezo mingine ndani na nje ya Tanzania.

Edtior's Picks

Latest Articles

Sportsleo Bongo Developed and designed by Mediapix Limited