Nyota wa kimataifa wa Kenya Abdallah Hassan ameachana na klabu ya Coastal Union baada ya kufikia makubaliano ya Pande zote mbili.
Mshambuliaji huyo aliyesajiliwa wakati wa dirisha dogo la usajili mwezi Januari ameondoka hapo baada ya kukubaliana na mabosi wa klabu hiyo kuvunja mkataba huo.
Huyu anakuwa mchezaji wa pili kutoka Kenya kuachana na Coastal Union baada ya John Makwata ambaye alitimka mapema wakati wa dirisha dogo huku ikielezwa kuwa sababu ni kushindwa kutekeleza baadhi ya makubaliano ya mikataba ambayo walikubaliana.
Coastal union imekua ikisajili mastaa mbalimbali ili kufanya vizuri katika ligi kuu ya Nbc nchini chini ya kocha Juma Mwambusi japo sasa kukaa na mastaa hao imekua changamoto.
🎯 Usipitwe!
Kuwa wa kwanza kupata habari za moto za michezo nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, moja kwa moja kwenye barua pepe yako kutoka SportsLeo Bongo!
- ✅ Matokeo ya mechi
- ✅ Uchambuzi wa kina
- ✅ Habari za ndanii ya timu zako pendwa
✉️ Quality content, no spam. Unsubscribe anytime.
Mpaka sasa katika msimamo wa ligi kuu ya Nbc nchini ipo nafasi ya tisa ikiwa na alama 25 baada ya kucheza michezo 23.