Kocha mkuu wa Simba Sc,Sven Vandenbroeck amekanusha taarifa zilizoenea mtandaoni kuhusu nyota wake namba moja Meddie Kagere kuwa walipigana.
Sven amesema kuwa taarifa hizo si za kweli na hawezi kutumia nguvu kulizungumzia hilo kwakuwa halina maana kwani hajui wapi lilipotokea hadi kuzuka mitandaoni.
“Ninaloweza kusema ni kuwa sina tatizo na Meddie Kagere”alisema Sven baada yakutotaka mahojiano marefu.