Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars, Etienne Ndayiragije amesema kuwa teknolojia mpya inayotumika ndani ya timu hiyo kwa sasa itarahisisha kazi kwani ataweza kutambua muda na uwezo wa wachezaji wake wakati wa mazoezi.
Ndayiragije amesema kuwa kwa sasa wachezaji wanatumia vifaa maalumu ambavyo wanavivaa (GPS) wakiwa mazoezini, vifaa hivyo vitasaidia kutambua utimamu wa mwili kwa wachezaji wake.
“Vifaa wanavyovaa vimekuwa vikitumiwa pia na wachezaji wakubwa katika kufanya kwao mazoezi hiki ni kitu kizuri na nina imani kitakuwa na matokeo chanya kwani vinasaidia kutambua utimamu wa mwili pamoja na uwezo wao kwa muda ambao wamefanya mazoezi”alisema Ndayiragije